Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasim Majaliwa ampongeza Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) Bi.Christine Mwakatobe kwa kutoa huduma bora za kumbi za mikutano nchini.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri Mkuu wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kikao Kazi cha tathmini ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa Mwaka wa Fedha 2024/20025 kilichofanyika katika Ukumbi wa Simba AICC, jijini Arusha tJulai 8, 2025.
Uongozi wa AICC unaendelea kufanya mageuzi makubwa ya kutoa huduma zenye viwango vya kimataifa ili kukidhi mahitaji ya stahiki katika sekta ya utalii wa mikutano.
Hatua zinazochukuliwa ni pamoja na ukarabati wa kumbi za mikutano, kufunga vifaa vya kisasa vya TEHAMA, vifaa vya kutafsiri lugha mbalimbali na kutumia watumishi wa AICC waliobobea katika utalii wa mikutano.