THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

ARUSHA INTERNATIONAL CONFERENCE CENTRE

Wafanyakazi AICC Watakiwa Kuongeza Bidii Katika Utendaji

Wafanyakazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) wametakiwa kuogeza bidii katika kufanya kazi ili Kituo kiendelee kuongeza mapato zaidi katika kutoa huduma za utalii wa mikutano nchini.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Bi. Christine G. Mwakatobe, leo tarehe 3 Februari 2026 alipokutana na wafanyakazi kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya kukiendeleza kituo na kijipanga vyema kwa mwaka 2026.
Katika mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya AICC jijini Arusha, Bi. Mwakatobe amesema kila mtu akijituma kwa nafasi yake katika kuhudumia wateja, AICC itaendelea kupiga hatua kubwa ya ufanisi kadri muda unavyosogea.
Vile vile, amechukua nafasi hiyo kutoa pongezi za dhati kwa Menejimenti na Watumishi wote kwa weledi na jitihada zilizopelekea mafanikio makubwa ya kiutendaji kwa mwaka uliopita, huku akisisitiza azma ya kuzidisha huduma kwa wateja.
AICC pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kilichopo jijini Dar es Salaam vimeendelea kutoa huduma za mikutano ya kimataifa na kikanda hali ambayo imeonesha utayari na uwezo wa kuhudumia mikutano ya kiwango hicho.

Facebook
X
LinkedIn

Event Booking Request