News
Maandalizi Mkutano IPU Umefikia Pazuri RC.CPA.Makalla
Details
Maandalizi yanayofanywa na Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano Arusha (AICC) kwa ajili ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa
Mabunge Duniani (IPU) yamefikia pazuri kutokana na kazi nzuri
inayofanywa na AICC hadi sasa.
Akizungumza Jana, Septemba 18, 2026 jijini Arusha, Kituoni hapo wakati wa ziara ya kukagua maandalizi na ukarabati, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. CPA. Amos Makalla ameeleza kuridhishwa kwake na mabadiliko makubwa yaliyofanyika kwa ufasaha na ndani ya muda mfupi. Mkuu huyo amethibitisha kuwa kituo hicho pamoja na Mkoa wa Arusha viko tayari kuwa mwenyeji wa Mkutano huo wa kipekeee.
Amefafanua zaidi kuwa Mkutano huo unatarajiwa kukutanisha zaidi ya mataifa 185 duniani kote na utaleta heshima kubwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan, pamoja na taifa zima kwa ujumla.
Vilevile, Mhe. Makalla amelishukuru Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano wa karibu lililotoa katika kipindi chote cha maandalizi, huku akibainisha kuwa hivi sasa zimesalia asilimia chache tu ili kukamilisha 100 asilimia.
Published Date:
September 18, 2026