THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

ARUSHA INTERNATIONAL CONFERENCE CENTRE

MKUTANO MKUU WA TATHMINI YA UTEKELEZAJI KAZI NUSU MWAKA WA FEDHA 2025/2026

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar leo Januari 5, amewasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho, Bi. Christine Mwakatobe. 🤝✨
Akiwa kituoni hapo, Mhe. Waziri amefungua Mkutano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) unaofanyika katika ukumbi wa Simba, ukilenga kufanya tathmini ya utendaji wa kazi kwa kipindi cha nusu mwaka.
Katika ziara hiyo, Mhe. Balozi Khamis ameambatana na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mshamu Ali Munde, pamoja na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula.
Arusha inaendelea kuwa kitovu cha mikutano ya kimkakati!
#AICC #Arusha #TRA #WizaraYaFedha #Maendeleo #MkutanoWaTathmini #Tanzania #DiplomasiaYaMikutano

Facebook
X
LinkedIn

Event Booking Request