Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman amefunga rasmi Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika, leo Julai 11, 2025 unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), jijini Arusha.
Mkutano huo wa siku 2 ulifunguliwa rasmi jana Julai 10, 2025 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango