Jana, Februari 18,2026, Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Moses Mpogole Kusiluka, amefungua rasmi Kikao Kazi cha Sita cha Mwaka cha Serikali Mtandao (e-GA) katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha(Aicc)
“Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye TEHAMA kwa kutambua kuwa maendeleo ya sasa hayawezi kupatikana nje ya mifumo ya kidijitali” Amesema Mhe. Kusiluka
Mafanikio ya Tanzania katika nyanja hii yameendelea kung’ara kimataifa, ambapo Mhe. Balozi ametoa pongezi za dhati kwa bodi, menejimenti, na wadau wote wa e-GA kwa kazi nzuri iliyopelekea nchi yetu kutambuliwa na kutunukiwa tuzo ya kimataifa ya Huduma za Umma ya Umoja wa Mataifa (United Nations Public Service Award). Tuzo hii ni ushahidi tosha kuwa Tanzania ipo katika mwelekeo sahihi wa mageuzi ya kidijitali yanayozingatia weledi, ufanisi, na viwango vya juu vya kimataifa katika utoaji wa huduma kwa umma.
Kwa siku hizi tatu za kikao kazi, matarajio ni kuona washiriki wakitumia jukwaa hili kubuni na kuja na masuluhisho yatakayoleta tija zaidi badala ya uharibifu. Ni wakati wa kuwa na mtazamo chanya na kuwekeza kwenye matumizi sahihi ya TEHAMA katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ili kufikia malengo ya nchi.