KONGAMANO LA 5 LA IDHAA ZA KISWAHILI DUNIANI

Arusha, Machi 24, 2026 – Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, leo amefungua rasmi Kongamano la 5 la Idhaa za Kiswahili Duniani katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC). Akizungumza katika hafla ya ufunguzi, Mhe. Abdulla ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, akiwataja kama vinara wa mshikamano, maendeleo na mabalozi mahiri wa Kiswahili ndani na nje ya Tanzania. Aidha, amelitambua jukumu kubwa la Baraza la Kiswahili Tanzania na Baraza la Kiswahili Zanzibar kwa kuratibu kongamano hilo, akisisitiza kuwa Kiswahili ni nguzo ya utambulisho, mshikamano na diplomasia ya kikanda na kimataifa. Katika hotuba yake, Mhe. Abdulla amewataka waandishi wa habari na wadau wa Kiswahili kutumia teknolojia za kisasa ili kufikisha lugha hiyo kwa hadhira pana zaidi duniani. Amesisitiza nafasi ya vijana katika mustakabali wa Kiswahili kupitia ubunifu wa kidijitali, ikiwemo maudhui ya mitandao ya kijamii, video za elimu na programu za simu. Ameeleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zitaendelea kuunga mkono juhudi za kukuza Kiswahili kwa kuimarisha mafunzo ya ubunifu wa kidijitali, kuwezesha mitaji, kuboresha miundombinu ya TEHAMA na kushirikiana na sekta binafsi
Benki ya Azania Yaongeza Chachu Huduma za Kifedha AICC Arusha

Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kimeingia katika awamu mpya ya maboresho ya huduma kwa wateja wake baada ya Benki ya Azania kuzindua rasmi huduma za ATM ndani ya kituo hicho leo 16.03.2026, hatua inayolenga kurahisisha miamala kwa washiriki wa mikutano ya ndani na ya ya kimataifa. Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa huduma hiyo , Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa AICC, Bi. Christine Mwakatobe, amesema uwepo wa huduma hiyo ni suluhisho la kimkakati katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma za kifedha iliyokuwa ikiwakabili wadau na wageni wa kituo hicho. “Biashara yetu kuu hapa AICC ni mikutano ya kimataifa na kitaifa. Uwepo wa ATM hii utatatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya upatikanaji wa huduma za kifedha na kurahisisha miamala kwa wageni wetu wanaotoka kila pembe ya dunia,” amesema Bi. Mwakatobe. Vile vile, Bi. Mwakatobe ameupongeza uongozi wa benki hiyo kwa mwitikio wao wa haraka na ushirikiano uliowezesha huduma hiyo kuanza kutolewa. Aliongeza kuwa AICC itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha pande zote mbili zinanufaika kikamilifu na uwekezaji huo. Uzinduzi huu ni sehemu ya jitihada za AICC kuendelea kuwa kituo bora cha mikutano barani Afrika kwa kutoa huduma jumuishi na rafiki kwa wateja na sekta ya mikutano.
SALAMU ZA PONGEZI

Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Watumishi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) tunakupongeza Mhe. Bal. Steven P. Mbundi kwa kuchaguliwa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Africa Mashariki kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tunakuahidi ushirikiano katika kutekeleza majukumu yako.
Mageuzi ya Kidijitali kwa Ustawi wa Taifa: Kikao Kazi cha 6 cha Serikali Mtandao (e-GA) Chafunguliwa Arusha 🇹🇿

Jana, Februari 18,2026, Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Moses Mpogole Kusiluka, amefungua rasmi Kikao Kazi cha Sita cha Mwaka cha Serikali Mtandao (e-GA) katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha(Aicc) “Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye TEHAMA kwa kutambua kuwa maendeleo ya sasa hayawezi kupatikana nje ya mifumo ya kidijitali” Amesema Mhe. Kusiluka Mafanikio ya Tanzania katika nyanja hii yameendelea kung’ara kimataifa, ambapo Mhe. Balozi ametoa pongezi za dhati kwa bodi, menejimenti, na wadau wote wa e-GA kwa kazi nzuri iliyopelekea nchi yetu kutambuliwa na kutunukiwa tuzo ya kimataifa ya Huduma za Umma ya Umoja wa Mataifa (United Nations Public Service Award). Tuzo hii ni ushahidi tosha kuwa Tanzania ipo katika mwelekeo sahihi wa mageuzi ya kidijitali yanayozingatia weledi, ufanisi, na viwango vya juu vya kimataifa katika utoaji wa huduma kwa umma. Kwa siku hizi tatu za kikao kazi, matarajio ni kuona washiriki wakitumia jukwaa hili kubuni na kuja na masuluhisho yatakayoleta tija zaidi badala ya uharibifu. Ni wakati wa kuwa na mtazamo chanya na kuwekeza kwenye matumizi sahihi ya TEHAMA katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ili kufikia malengo ya nchi.
SERIKALI YASISITIZA UIMARISHAJI WA KINGA YA JAMII KULINDA USTAWI WA WATANZANIA

Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kusisitiza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya kinga ya jamii ili kulinda ustawi wa Watanzania. Akifungua rasmi Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Kinga ya Jamii leo, Februari 9, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Deus Clement Sangu, amesema kuwa “Kinga ya jamii ni haki ya msingi ya binadamu” inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa (UN) pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO). Mhe. Sangu amebainisha kuwa Serikali chini ya uongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta hii, ikilenga kuimarisha mifumo ya kisheria na kifedha ili kuwalinda wananchi dhidi ya changamoto kama magonjwa, ulemavu na ukosefu wa kipato. “Ni wajibu wa wadau kutumia mkutano huu wa siku mbili kuibua mikakati thabiti itakayohakikisha kila mwananchi ananufaika na mifumo hii kwa tija,” alisema Mhe. Sangu. Mkutano huo uliobeba kauli mbiu ya “Kinga ya Jamii kwa Wote Msingi wa Maendeleo”umewakutanisha watunga sera na wadau wa maendeleo kwa lengo la kutathmini mafanikio yaliyopatikana na kuweka mwelekeo mpya wa kuwafikia wananchi wengi zaidi.
KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI

AICC inaiheshimisha Tanzania ndani na nje ya nchi, Mhe. CPA. Amos Gabriel Makala Mkuu wa Mkoa wa Arusha
TANGAZO LA MNADA WA HADHARA

MKURUGENZI WA KITUO CHA KIMATAIFA CHA MIKUTANO ARUSHA (AICC) ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA KUTAKUWA NA MNADA WA HADHARA WA VIFAA MBALIMBALI VILIVYOTOKANA NA MAJENGO YALIYOBOMOLEWA. MNADA HUO UTAFANYIKA TAREHE 09 FEBRUARI 2026 KUANZIA SAA 4.00 ASUBUHI MAENEO YA KOTA ZA AICC KIJENGE, ILIPOKUWA AICC CLUB. VIFAA VITAKAVYOPIGWA MNADA NI: MILANGO, FREMU ZA MILANGO, MADIRISHA, GRILI ZA MILANGO NA MAGETI, MBAO, MABATI, MITI NA MAGOGO, KWA UCHACHE VIMETAJWA. MASHARTI YA MNADA: a. KIFAA KITAUZWA KAMA KILIVYO NA MAHALI KILIPO;b . ATAKAYETAJA BEI YA JUU KABLA YA NYUNDO KUGONGWA NDIYE ATAKAYEUZIWA KIFAA;c. ALIYETAJA BEI YA JUU SIO LAZIMA AUZIWE KAMA BEI HIYO HAIJAFIKIA BEI ILIYOTARAJIWA;d. MNUNUZI ATATAKIWA KULIPIA PESA YOTE PAPO HAPO (ASILIMIA MIA MOJA), AKISHINDWA KULIPIA KIFAA HICHO KITANADIWA UPYA;e. MNUNUZI ATATAKIWA KUCHUKUA KIFAA CHAKE SIKU HIYO HIYO;f. SIKU YA KUKAGUA VIFAA HIVYO NI TAREHE 07.02.2026 KUANZIA SAA 3.00 ASUBUHI HADI SAA 9.00 ALASIRI. Tarehe ya mnada utakaofuata itatangazwa mwisho wa mnada wa tarehe 09 Februari 2026 IMETOLEWA NA UONGOZI Limetolewa Tarehe 17 Januari 2026
Wafanyakazi AICC Watakiwa Kuongeza Bidii Katika Utendaji

Wafanyakazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) wametakiwa kuogeza bidii katika kufanya kazi ili Kituo kiendelee kuongeza mapato zaidi katika kutoa huduma za utalii wa mikutano nchini.Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Bi. Christine G. Mwakatobe, leo tarehe 3 Februari 2026 alipokutana na wafanyakazi kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya kukiendeleza kituo na kijipanga vyema kwa mwaka 2026.Katika mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya AICC jijini Arusha, Bi. Mwakatobe amesema kila mtu akijituma kwa nafasi yake katika kuhudumia wateja, AICC itaendelea kupiga hatua kubwa ya ufanisi kadri muda unavyosogea.Vile vile, amechukua nafasi hiyo kutoa pongezi za dhati kwa Menejimenti na Watumishi wote kwa weledi na jitihada zilizopelekea mafanikio makubwa ya kiutendaji kwa mwaka uliopita, huku akisisitiza azma ya kuzidisha huduma kwa wateja.AICC pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kilichopo jijini Dar es Salaam vimeendelea kutoa huduma za mikutano ya kimataifa na kikanda hali ambayo imeonesha utayari na uwezo wa kuhudumia mikutano ya kiwango hicho.
Wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Watumishi wa kituo cha kimataifa cha mikutano Arusha (AICC). Tunawatakia kheri wazanzibari wote kwa kuadhimisha miaka 62 ya mapinduzi ya zanzibar.
AICC at Zanzibar International Trade Fair

Assah Mwambene, the Principal Customer Relations at Arusha International Conference Centre speaks to visitors at the Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation Pavilion yesterday at the ongoing Zanzibar International Trade Fair.