Mageuzi ya Kidijitali kwa Ustawi wa Taifa: Kikao Kazi cha 6 cha Serikali Mtandao (e-GA) Chafunguliwa Arusha 🇹🇿

Jana, Februari 18,2026, Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Moses Mpogole Kusiluka, amefungua rasmi Kikao Kazi cha Sita cha Mwaka cha Serikali Mtandao (e-GA) katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha(Aicc) “Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye TEHAMA kwa kutambua kuwa maendeleo ya sasa hayawezi kupatikana nje ya mifumo ya kidijitali” Amesema Mhe. Kusiluka Mafanikio ya Tanzania katika nyanja hii yameendelea kung’ara kimataifa, ambapo Mhe. Balozi ametoa pongezi za dhati kwa bodi, menejimenti, na wadau wote wa e-GA kwa kazi nzuri iliyopelekea nchi yetu kutambuliwa na kutunukiwa tuzo ya kimataifa ya Huduma za Umma ya Umoja wa Mataifa (United Nations Public Service Award). Tuzo hii ni ushahidi tosha kuwa Tanzania ipo katika mwelekeo sahihi wa mageuzi ya kidijitali yanayozingatia weledi, ufanisi, na viwango vya juu vya kimataifa katika utoaji wa huduma kwa umma. Kwa siku hizi tatu za kikao kazi, matarajio ni kuona washiriki wakitumia jukwaa hili kubuni na kuja na masuluhisho yatakayoleta tija zaidi badala ya uharibifu. Ni wakati wa kuwa na mtazamo chanya na kuwekeza kwenye matumizi sahihi ya TEHAMA katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ili kufikia malengo ya nchi.
SERIKALI YASISITIZA UIMARISHAJI WA KINGA YA JAMII KULINDA USTAWI WA WATANZANIA

Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kusisitiza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya kinga ya jamii ili kulinda ustawi wa Watanzania. Akifungua rasmi Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Kinga ya Jamii leo, Februari 9, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Deus Clement Sangu, amesema kuwa “Kinga ya jamii ni haki ya msingi ya binadamu” inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa (UN) pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO). Mhe. Sangu amebainisha kuwa Serikali chini ya uongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta hii, ikilenga kuimarisha mifumo ya kisheria na kifedha ili kuwalinda wananchi dhidi ya changamoto kama magonjwa, ulemavu na ukosefu wa kipato. “Ni wajibu wa wadau kutumia mkutano huu wa siku mbili kuibua mikakati thabiti itakayohakikisha kila mwananchi ananufaika na mifumo hii kwa tija,” alisema Mhe. Sangu. Mkutano huo uliobeba kauli mbiu ya “Kinga ya Jamii kwa Wote Msingi wa Maendeleo”umewakutanisha watunga sera na wadau wa maendeleo kwa lengo la kutathmini mafanikio yaliyopatikana na kuweka mwelekeo mpya wa kuwafikia wananchi wengi zaidi.
KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI

AICC inaiheshimisha Tanzania ndani na nje ya nchi, Mhe. CPA. Amos Gabriel Makala Mkuu wa Mkoa wa Arusha
TANGAZO LA MNADA WA HADHARA

MKURUGENZI WA KITUO CHA KIMATAIFA CHA MIKUTANO ARUSHA (AICC) ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA KUTAKUWA NA MNADA WA HADHARA WA VIFAA MBALIMBALI VILIVYOTOKANA NA MAJENGO YALIYOBOMOLEWA. MNADA HUO UTAFANYIKA TAREHE 09 FEBRUARI 2026 KUANZIA SAA 4.00 ASUBUHI MAENEO YA KOTA ZA AICC KIJENGE, ILIPOKUWA AICC CLUB. VIFAA VITAKAVYOPIGWA MNADA NI: MILANGO, FREMU ZA MILANGO, MADIRISHA, GRILI ZA MILANGO NA MAGETI, MBAO, MABATI, MITI NA MAGOGO, KWA UCHACHE VIMETAJWA. MASHARTI YA MNADA: a. KIFAA KITAUZWA KAMA KILIVYO NA MAHALI KILIPO;b . ATAKAYETAJA BEI YA JUU KABLA YA NYUNDO KUGONGWA NDIYE ATAKAYEUZIWA KIFAA;c. ALIYETAJA BEI YA JUU SIO LAZIMA AUZIWE KAMA BEI HIYO HAIJAFIKIA BEI ILIYOTARAJIWA;d. MNUNUZI ATATAKIWA KULIPIA PESA YOTE PAPO HAPO (ASILIMIA MIA MOJA), AKISHINDWA KULIPIA KIFAA HICHO KITANADIWA UPYA;e. MNUNUZI ATATAKIWA KUCHUKUA KIFAA CHAKE SIKU HIYO HIYO;f. SIKU YA KUKAGUA VIFAA HIVYO NI TAREHE 07.02.2026 KUANZIA SAA 3.00 ASUBUHI HADI SAA 9.00 ALASIRI. Tarehe ya mnada utakaofuata itatangazwa mwisho wa mnada wa tarehe 09 Februari 2026 IMETOLEWA NA UONGOZI Limetolewa Tarehe 17 Januari 2026
Wafanyakazi AICC Watakiwa Kuongeza Bidii Katika Utendaji

Wafanyakazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) wametakiwa kuogeza bidii katika kufanya kazi ili Kituo kiendelee kuongeza mapato zaidi katika kutoa huduma za utalii wa mikutano nchini.Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Bi. Christine G. Mwakatobe, leo tarehe 3 Februari 2026 alipokutana na wafanyakazi kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya kukiendeleza kituo na kijipanga vyema kwa mwaka 2026.Katika mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya AICC jijini Arusha, Bi. Mwakatobe amesema kila mtu akijituma kwa nafasi yake katika kuhudumia wateja, AICC itaendelea kupiga hatua kubwa ya ufanisi kadri muda unavyosogea.Vile vile, amechukua nafasi hiyo kutoa pongezi za dhati kwa Menejimenti na Watumishi wote kwa weledi na jitihada zilizopelekea mafanikio makubwa ya kiutendaji kwa mwaka uliopita, huku akisisitiza azma ya kuzidisha huduma kwa wateja.AICC pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kilichopo jijini Dar es Salaam vimeendelea kutoa huduma za mikutano ya kimataifa na kikanda hali ambayo imeonesha utayari na uwezo wa kuhudumia mikutano ya kiwango hicho.
Wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Watumishi wa kituo cha kimataifa cha mikutano Arusha (AICC). Tunawatakia kheri wazanzibari wote kwa kuadhimisha miaka 62 ya mapinduzi ya zanzibar.
AICC at Zanzibar International Trade Fair

Assah Mwambene, the Principal Customer Relations at Arusha International Conference Centre speaks to visitors at the Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation Pavilion yesterday at the ongoing Zanzibar International Trade Fair.
MKUTANO MKUU WA TATHMINI YA UTEKELEZAJI KAZI NUSU MWAKA WA FEDHA 2025/2026

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar leo Januari 5, amewasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho, Bi. Christine Mwakatobe. 🤝✨ Akiwa kituoni hapo, Mhe. Waziri amefungua Mkutano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) unaofanyika katika ukumbi wa Simba, ukilenga kufanya tathmini ya utendaji wa kazi kwa kipindi cha nusu mwaka. Katika ziara hiyo, Mhe. Balozi Khamis ameambatana na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mshamu Ali Munde, pamoja na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula. Arusha inaendelea kuwa kitovu cha mikutano ya kimkakati! #AICC #Arusha #TRA #WizaraYaFedha #Maendeleo #MkutanoWaTathmini #Tanzania #DiplomasiaYaMikutano
Tanzania’s MICE Revolution

Tanzania is swiftly emerging as one of Africa’s most exciting destinations for Meetings, Incentives, Conferences, and Exhibitions (MICE). It’s not just about hosting events, it’s about creating unforgettable experiences where business seamlessly blends with adventure. Whether it’s in the dynamic conference halls of Dar es Salaam or amidst the awesome landscapes of Zanzibar and the Serengeti, Tanzania offers a unique combination of business and leisure, making it Africa’s next great MICE destination. Solid Infrastructure to Support Growth Tanzania’s rise as a premier MICE destination is built on a foundation of solid infrastructure. Hosting international conferences requires more than just a few good hotels and reliable Wi-Fi—it demands purpose-built venues, modern technology, and excellent connectivity. Tanzania has invested significantly in these areas to meet global standards. The Julius Nyerere International Conference Centre (JNICC) in Dar es Salaam is one of the country’s most modern and largest venues, accommodating up to 1,000 delegates. The Arusha International Conference Centre (AICC) is another key asset, offering a prime location in the heart of East Africa, ideal for regional and international events and meetings. These venues provide flexible spaces, cutting-edge technology, and services tailored to meet the needs of both large-scale conventions and smaller, more intimate executive conferences. Additionally, Tanzania’s government is actively developing its transport infrastructure. The country’s roads, airports, and rail networks are all being expanded, making travel within and to Tanzania seamless for international delegates. With major upgrades to Julius Nyerere International Airport and the growing capacity of Kilimanjaro International Airport, Tanzania is increasingly becoming a hub for business events in East Africa.  Aviation Connectivity and the Role of PCOs and DMCs Aviation connectivity is another critical factor that sets Tanzania apart as a MICE destination. Julius Nyerere International Airport, handling around 4.5 million passengers annually, connects Tanzania to major business hubs in Africa, Europe, and the Middle East. Direct flights to cities like Dubai, Heathrow, Amsterdam, Nairobi, and Addis Ababa ensure that international delegates can access Tanzania with ease.  Kilimanjaro International Airport is another vital link for regional MICE events. Tanzania’s central location in East Africa makes it easily accessible for delegates across the continent. The government’s ongoing investment in airport infrastructure and expanded flight routes is only set to improve Tanzania’s competitive edge and comparative advantage in the global MICE sector. However, a successful MICE experience goes beyond just great venues and connectivity. The role of Professional Conference Organizers (PCOs) is to support event planning and organisations, especially in addressing the local content supply side for roles like interpretation, exhibitions, and conference moderation makes conferences benefit and an endless number of prayers. Destination Management Companies (DMCs), such as companies, tour guides, hotels, and culinary facilities provide conference delegates with an unforgettable experience. These professionals handle all aspects of event planning, from logistical coordination to local tours and entertainment, ensuring that each conference or meeting is tailored to meet both business goals and the interests of delegates. PCOs and DMCs in Tanzania manage around 90% of the overall event budget, handling everything from delegate registration and transportation to organizing cultural excursions, tours, and even local entertainment. It is estimated that, an average MICE tourists spend about 420USD per day for accommodation, conferences, eating, buying souvenirs, and other recreation, while 10% goes to event facilities. For large-scale conferences, these professionals often account for a significant portion of the economic impact, with the potential to generate upwards of 2 billion Tshs in direct business from a single event. These service providers ensure that delegates have an experience that goes beyond the conference room, deepening their connection with the country and leaving a lasting impression of Tanzania as a business hub.
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa AICC wakifuatilia kwa karibu kukao hicho kilichofanyika Makao Makuu ya AICC jijini Arusha.

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa AICC wakifuatilia kwa karibu kukao hicho kilichofanyika Makao Makuu ya AICC jijini Arusha. The AICC’s First Annual General Meeting participants following up the session during that  meeting held at the AICC Headquarters in Arusha city.