Ikiwa ni hatua muhimu ya maandalizi ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, leo 24.04.2026 Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Baraka Leonard amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Balozi Dkt. Jilly Maleko ofisini kwake Jijini Dodoma akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Bi. Christine Mwakatobe.
Mazungumzo hayo yamejikita katika kuangalia maandalizi ya mkutano huo ambapo Tanzania kupitia AICC imejipanga vilivyo kuwa mwenyeji wa mkutano huo kwani maadalizi tayari yameanza. Aidha, mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Bunge Bw. Daniel Eliufoo na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa AICC Dkt. Philip Chitaunga.