AICC tano bora ( 5 ), mashirika yenye ufanisi , matumizi na mapato na rejesho la mtaji. Katika kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma, Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu ameipongeza AICC kwa kuwa miongoni mwa mashirika matano bora nchini kwa ufanisi, matumizi bora ya rasilimali na mapato yenye tija kwa maendeleo ya taifa.” Pongezi hizo zilitolewa wakati wa Kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), jijini Arusha.