Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AICC wametembelea baadhi ya miradi ya AICC

Pichani Mkurugenzi Mkuu wa AICC Bwana Ephraim Mafuru akiwaongoza wajumbe wa Bodi ya AICC kujionea kazi ya maboresho inayoendelea kituoni hapa.

Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AICC leo( tarehe 10/06/2023) wametembelea baadhi ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Kituo hicho Cha Kimataifa Cha Mikutano jijini Arusha.Miradi waliyotembelea ni pamoja na Upanuzi wa Vyumba vya Mikutano AICC makao makuu na uboreshaji wa hospitali ya AICC.Maboresho ya miradi hiyo ya kimkakati yaliridhiwa na Bodi hiyo inayoendelea na vikao vyake jijini Arusha
Lengo la kuboresha miradi hiyo ni kuongeza mapato ya AICC.

en_USEnglish
X