NAIBU WAZIRI MKUU AFUNGA MKUTANO WA AGRF 2023

Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amehutubia katika Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2023 (AGRF 2023). Dkt. Biteko amemuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa katika Jukwaa hilo ambalo limefikia tamati leo Septemba 8, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tanzania.

en_USEnglish
X