Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Kimataifa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) jana alikutana na Jumuiya ya Kimataifa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam kutoa ufafanuzi juu ya kinachoendelea eneo la Ngorongoro na kusisitiza kuwa sheria za kimataifa za haki za binadamu zinatekelezwa ipasavyo ambapo wananchi wanahama kwa ridhaa yao wenyewe.

en_USEnglish
X