Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

RASIMU YA AICC KATIKA HOTUBA YA BAJETI 2023

Na Freddy Maro

Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Dkt.Stergomena Tax amesema mpango mkakati wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha wa kujenga kituo  kikubwa zaidi cha kisasa cha mikutano jijini humo  kutaiwezesha AICC kutekeleza kwa ufanisi jukumu lake la kukuza na kuendeleza diplomasia ya Mikutano   kutalipatia taifa fedha nyingi za kigeni.

Waziri Tax alisema hayo oleo wakati akisoma hotuba bajeti ya wizara yake Bungeni jijini Dodoma leo.

“Kituo kilikamilisha andiko la Biashara la mradi wa Mount Kilimanjaro International Convention Centre (MK-ICC) na kuliwasilisha Wizara ya Fedha na Mipangoambapo AICC imepata kibali cha kuendelea na mradi huo kwa njia ya Ubia na Sekta Binafsi. Ujenzi wa Kituo hicho kutaimarisha na kuongeza kasi ya utekelezaji wa diplomasia ya mikutano na maonesho hapa nchini, pamoja na kuongeza mapato ya fedha za kigeni,”alisema.

 Dr. Tax aliliambia bunge kwamba kipindi cha Mwaka wa Fedha 2022/2023 Kituo(AICC)  kilipanga kukusanya mapato ya Shilingi 16,737,049,856. Hadi mwezi Aprili, 2023 Kituo kilikusanya mapato ya Shilingi 12,782,629,220 sawa na asilimia 76 ya malengo.

“ Mapato hayo yalitokana na huduma za kumbi za mikutano (AICC na JNICC) shilingi 6,582,450,243; upangishaji wa ofisi na nyumba za kuishi shilingi 3,255,585,561; na huduma za hospitali shilingi 3,170,304,225. 153.”alisema.

Wakati wa hotuba yake Waziri huyo alibainisha kuwa kati ya mwezi Julai, 2022 hadi Aprili, 2023 AICC ilihudumia mikutano 399 ya kitaifa, na 21 ya kimataifa, ambayo ilileta washiriki 109,582 wa kitaifa, na 7,849 wa kimataifa; kimehudumia wagonjwa wa nje wapatao 71,220 na wagonjwa waliolazwa 1,300.

Dr. Tax aliongeza kusema kuwa AICC  imeandaa mifumo ya kielektroniki kama, Human Capital Management Information System (HCMIS), e-Office pamoja na kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya shughuli za mikutano.

“Katika kipindi hicho AICC ilifanya ukarabati wa nyumba 145 92 za makazi katika miliki za kituo zilizoko katikati ya jiji la Arusha; ukarabati wa ofisi, kumbi na hospitali; pamoja na kukamilisha mpango wa mafunzo na zoezi la kuhuisha muundo wa utumishi,”alisema.

Kwa kuzingatia sheria iliyoanzisha Kituo Cha Kimataifa cha Mikutano Arusha( AICC) inatekeleza majukumu yake kwa kuongozwa na Mpango Mkakati wa miaka mitano (2022/23 – 2026/27).

 Mpango huo unaainisha dira na dhima ya Kituo, hususan katika kuitangaza nchi yetu katika nyanja ya utalii wa mikutano na matukio (business tourism) ambayo inajulikana kama “MICE” (Meetings, Incentive travel, Conferences, Exhibition/Events).

AICC iliundwa mwaka 1978 baada ya kuvunjika iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977 ikiwa na jukumu la kukuza na kuendeleza utalii wa Mikutano nchini pamoja na kutunza na kuendeleza nyumba za kupanga, ofisi na hospitali zilizopo jijini Arusha.AICC pia inamiliki na kuendesha Kituo kingine cha Kimtaifa cha Mikutano cha Julius Nyerere International Convention Centre(JNICC) kilichopo jijini Dar es Salaam.

AICC ni shirika la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia mia moja na lipo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mwisho


 

en_USEnglish
X